Awali niliweka mtiririko kadhaa kuonesha Namna Biblia inavyoelezea suala la #Uimbaji na #Utunzi wa Nyimbo Tak.
Leo nitaweka nyongeza ya mstari wa Biblia unaoelezea uwezo wa nyimbo/muziki mtakatifu kuleta uwepo na ufunuo wa Mungu mahali unapoimbwa,huu utakuwa Ni muendelezo wa tatu unaohusiana na ule wa kwanza na wa pili:
Rejea kitabu Cha "Mambo ya Nyakati.5:12-14.{2 Chronicles.5:12-14}.
Biblia imeandika;
"tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani, Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani Mia na ishirini wakipiga panda ;hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakasikizisha sauti moja ya kumsifu Mungu na Kumshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; NDIPO NYUMBA YA BWANA IKAJAWA NA WINGU, NAAM, NYUMBA YA BWANA, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; KWA KUWA NYUMBA YA MUNGU IMEJAA UTUKUFU WA BWANA."
Biblia ipo wazi kabisa, Mara Tu Baada ya waimbaji (na wapigaji-mstari wa 13) kuanza kazi yao NDIPO...nyumba ya Bwana ikajawa na Wingu(lililoashiria Utukufu wa Bwana-mstari wa 14).
Msisitizo Ni uleule...UPO UHUSIANO KATI YA;
•UIMBAJI(Kwaya na Nyimbo nyingine za Ibada), AU
• UTUNZI-(ukirejea mtiririko wa kwanza na wa pili),
PAMOJA NA UWEPO/UTUKUFU WA MUNGU PINDI nyimbo iliyotungwa ikiimbwa mahali husika.
*Suala Si KUTUNGA NYIMBO TU ama KUIMBA MYIMBO TU...SUALA NI:
"JE????UTUKUFU WA MUNGU UNAONEKANA PINDI NYIMBO HUSIKA INAPOWASILISHWA MAHALI?"
"Je???Nyimbo tunazotunga na kuimba zina NGUVU KIASI GANI KULETA MABADILIKO KWA MUIMBAJI NA MSIKILIZAJI?
*Mtiririko unaokuja nitaweka tafsiri ya mistari hapo juu kwa lugha ya Kiingereza(ili kuongeza upana wa maarifa) Kisha tutapata Uelewa na kinachomaanishwa.
nikutakie tafakari njema.
Anophrine D.S.
@Mzumbe University.
Comments
Post a Comment