Ndugu katika Kristo,Mwokozi wetu apewe sifa....
Leo tunaendelea na mtiririko wa pili(2) wa somo letu.Katika Mtiririko uliopita tulitoa utangulizi wa Neno kutoka kitabu cha "Kumbukumbu la Torati.31:19-22,30."
Leo nitatolea ufafanuzi kuhusu mistrari hii;
Jambo la umuhimu la kuona hapa ni kupitia mstari wa 19...Mungu anamwambia Musa "ANDIKA WIMBO HUU" ,katika Biblia ya kiingereza chepesi(Bible in Basic English) ,Neno lililotumika badala ya neno 'andika' ni neno 'tengeneza/kamilisha' ,Kutokana na hayo tuelewe yafuatayo;
>Ni jambo la muhimu kwa watunzi/waimbaji kutotengeneza wimbo/nyimbo kwa utaratibu tunaoutaka sisi Bali kwenda kwa gwiji wa Muziki Mtakatifu{ndiye Mungu mwenyewe},ili atupe wimbo/nyimbo yeye mwenyewe[kwa kuwa Musa aliambiwa "ANDIKA" ,Hakujiamulia peke yake].
Fahamu ya kuwa Nyimbo inayotoka kwa Mungu kwenda kwa mtunzi inabeba nguvu(upako) unaoelezewa katika mstari wa 21 kuwa;
(a)unakuwa SHAHIDI(ukishuhudia ndani ya anayeimba na kusikia).
(b)Unakaa katika kumbukumbu za anayeimba hadi wakati husika wa wimbo husika!
Ni tamaa ya Mungu kuwa tusiwe watunzi Tu!!Bali wabebaji wa sauti ya Mungu kupitia Muziki Mtakatifu.
"Mtunzi/Muimbaji ni MHUBIRI!!!"
"Uimbaji wa Nyimbo Tak. ni UHUBIRI!!"
Maana nyimbo Tak. Zatoka kwa Mungu...zatoka katika Biblia Tak.
-Hitimisho...#Mungu hutumia watunzi na waimbaji kusema na watu kama vile atumiavyo mapadre/wachungaji kusema na watu!!!
..."TUTUNGE NYIMBO TAK. KWA NGUVU ZAKE ALIYETUUMBA"
Comments
Post a Comment