Wapendwa katika Krisro Yesu ,Tumsifu Mwokozi wetu............... ~Kwa kitambo kirefu nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa ,likiwemo Hili ambalo nimeliweka kama kichwa cha muhtasari huu;'Biblia Takatifu inasema nini/inatufundisha vipi kuhusu utunzi[uandishi] wa nyimbo Takatifu?'. Hatimaye nimefanikiwa kupata mwangaza kidogo kulihusu jambo Hilo ,na majibu yake Ni ndani ya kitabu hikihiki tunachotembea nacho kila siku(Biblia Tak.). Nitatoa chambuzi hizi katika mfululizo wa masomo(vipindi)kadhaa na kwa kuanza na mtiririko wa kwanza nitakuonesha[ewe mtunzi wa nyimbo Tak.] mistari katika Biblia ,Kisha katika mtiririko wa pili nitaitolea ufafanuzi; Rejea 'Deutoronomy.31:19,21,22&30[Kumbukumbu la Torati.31:19,21,22&30] ,Biblia inasema;(nitatoa nukuu ya kiingereza na kiswahili pamoja): "And now write this song for yourselves and teach it to the Israelites;put it in their mouths, that this song may be a witness for me against the Israelites. And when many evil...
Comments
Post a Comment