Wapendwa katika Krisro Yesu ,Tumsifu Mwokozi wetu...............
~Kwa kitambo kirefu nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa ,likiwemo Hili ambalo nimeliweka kama kichwa cha muhtasari huu;'Biblia Takatifu inasema nini/inatufundisha vipi kuhusu utunzi[uandishi] wa nyimbo Takatifu?'.
Hatimaye nimefanikiwa kupata mwangaza kidogo kulihusu jambo Hilo ,na majibu yake Ni ndani ya kitabu hikihiki tunachotembea nacho kila siku(Biblia Tak.).
Nitatoa chambuzi hizi katika mfululizo wa masomo(vipindi)kadhaa na kwa kuanza na mtiririko wa kwanza nitakuonesha[ewe mtunzi wa nyimbo Tak.] mistari katika Biblia ,Kisha katika mtiririko wa pili nitaitolea ufafanuzi;
Rejea 'Deutoronomy.31:19,21,22&30[Kumbukumbu la Torati.31:19,21,22&30] ,Biblia inasema;(nitatoa nukuu ya kiingereza na kiswahili pamoja):
"And now write this song for yourselves and teach it to the Israelites;put it in their mouths, that this song may be a witness for me against the Israelites. And when many evils and troubles have befallen them ,this[sacred] song will confront them as a witness ,for it will never be forgotten from the mouths of their descendants.For I know their strong desire and the purpose which they are forming even now ,before I have brought them into the land which I swore to give them .Moses wrote this song the same day and taught It to the Israelites.And Moses spoke in the heearing of all the congregation of Israelites the words of this song until they were ended".(Amplified version).
Tafsiri ya kiswahili ya mistari hii Ni;
"Basi jiandikieni wimbo huu ,uwafundishe wana wa Israeli;ukawatie vinywani mwao ,ili uwe shahidi kwangu wimbo huu ,juu ya wana wa Israeli .Tena itakuwa wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka ,utashuhudia wimbo huu mbele Yao kama shahidi ,kwa maana hautasahaulika katika vinywa vya uzao wao;kwani nayajua mawazo Yao wayawazayo hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyowapa.Basi Musa akauandika wimbo huu siku iyo hiyo ,akawafundisha wana wa Israeli.Musa akasema maneno ya wimbo huu masikioni mwa kusanyiko la wana wa Israeli hata yakaisha".
Hiyo Ni mistari katika Biblia Takatifu ,katika mtiririko huu wa kwanza nimetaka tu kukuonesha hii mistari...katika mtiririko utakaofuata nitajaribu kuitolea ufafanuzi hii mistari ili tuone na kutambua wazi kuhusu Biblia Takatifu na Utunzi wa Muziki Mtakatifu(Hususani kwetu sisi watunzi).
Asante.!
Comments
Post a Comment