Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2016

Biblia Takatifu inasema nini kuhusu utunzi wa nyimbo Takatifu{Sacred songs}??!

Wapendwa katika Krisro Yesu ,Tumsifu Mwokozi wetu............... ~Kwa kitambo kirefu nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa ,likiwemo Hili ambalo nimeliweka kama kichwa cha muhtasari huu;'Biblia Takatifu inasema nini/inatufundisha vipi kuhusu utunzi[uandishi] wa nyimbo Takatifu?'. Hatimaye nimefanikiwa kupata mwangaza kidogo kulihusu jambo Hilo ,na majibu yake Ni ndani ya kitabu hikihiki tunachotembea nacho kila siku(Biblia Tak.). Nitatoa chambuzi hizi katika mfululizo wa masomo(vipindi)kadhaa na kwa kuanza na mtiririko wa kwanza nitakuonesha[ewe mtunzi wa nyimbo Tak.] mistari katika Biblia ,Kisha katika mtiririko wa pili nitaitolea ufafanuzi; Rejea 'Deutoronomy.31:19,21,22&30[Kumbukumbu la Torati.31:19,21,22&30] ,Biblia inasema;(nitatoa nukuu ya kiingereza na kiswahili pamoja): "And now write this song for yourselves and teach it to the Israelites;put it in their mouths, that this song may be a witness for me against the Israelites. And when many evil...

Tumsifu Yesu Kristo.........

Ni tumai langu kuwa nyote mu wazima ,Napenda kukukaribisha katika ukurasa huu, Ni wazo nililokuwa nalo toka kitambo ,kuanzisha ukurasa ambamo kupitia humo nitaweza kuweka mambo muhimu yanihusuyo kama vile nota za tunzi alizoniwezesha Mungu kuzitengeneza ,mashairi n.k ambayo yote kwa ujumla yanaweza kuwa ya msaada kwetu sote ili kulijenga kanisa la Mungu. Huu Ni mwanzo tu ,na taratibu ukurasa huu utakamilika hatua kwa hatua kadiri atakavyowezesha Roho Mtakatifu aliyeianzisha kazi hii. Asante! Anophrine Desdeus Shirima.